Aika "Tuliwasaidia Kina Rosa Ree, Wildad na Celine ili Watoke Kimuziki"


Baada ya kuwaibua Rosa Ree, Wildad na Seline kwenye kiwanda cha Bongo Fleva kupitia music lebel yao The Industry, Aika amesema kuwa kwa sasa hawatasimamia wasanii kama ilivyokuwa hapo awali na badala yake watatoa msaada tu kwa wasanii wenye vipaji na ukifika muda sahihi watatangaza nia yao ya kurudi tena kuwasimamia.

“Kweli tulifanya hivyo kama kutoa msaada kwa wasanii ambao hawana uwezo wakulipia gharama za studio na sasa hivi tumewaruhusu kila mmoja kufanyakazi zake wenyewe, hatuwezi kuwa-sign wasanii wengine sasa hivi badala yake tutaendelea kutoa msaada kwao ni kitu ambacho hatuwezi kuacha”- alisema @Aikanavykenzo

Member huyo wa kundi la NavyKenzo amesema, kwa sasa wamewekeza muda mwingi kwenye miradi ya kundi lao na ameahidi kurudi kuonekana tena kwenye majukwaa ya muziki sehemu tofauti nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad