Aishi Manula Mambo Yamkalia Vibaya Taifa Stars

Aishi Manula Mambo Yamkalia Vibaya Taifa Stars
KIPA namba moja wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula, jana alishindwa kujumuika na kikosi cha timu hiyo katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (Afcon) dhidi ya Uganda.



Manula ameshindwa kutokea katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko, Dar kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, Jumatatu iliyopita.



Meneja wa Taifa Stars, Danny Msangi amesema, Manula alijiunga na timu hiyo akiwa majeruhi lakini anaendelea na matibabu na wanaamini atakuwa sawa kabla ya kuvaana na Uganda.



“Madaktari wetu wanaendelea kupambana ili kuhakikisha anapona,” alisema Msangi.



Taifa Stars itapambana na Uganda, Septemba 8, huko Uganda na mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kuhitaji kushinda ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kutinga katika fainali hizo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad