Alichokisema Rammy Galis kwa Mtoto wa Masogange Baada ya Kumaliza Shule

Alichokisema  Rammy Galis kwa Mtoto wa Masogange Baada ya Kumaliza Shule
Mtoto wa marehemu Agnes Masogange, Sania Sabri Shabani amehitimu darasa la saba katika shule ya msingi Kisutu ikiwa baba yake mzazi ni miongoni waliohudhuria graduation yake iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii.

Muigizaji Rammy Galis aliamua kutumia ukurasa wake wa instagram kumpongeza Sania kwa kuhitimu shule ya msingi na kusema kuwa ataendelea kumpa support na asijihisi mpweke hata kama mama yake hayupo na amemuahidi kusimamia kipaji chake cha kuigiza.

Rammy Galis aliandika “Congratulations kwa kuhitimu shule ya msingi 🎈 #SANIYA , Mungu aendelee kukusimamia katika elimu yako , Sitakua nyuma katika hatua yako ya maendeleo . Sikuacha kuja kukutembelea shule alipokuwa hai marehm mama yako , Sitaacha kukupa pongezi ‘ bado haupo peke yako “

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad