Alikiba Aimwagia Fedha Coastal Union

Alikiba aimwagia fedha Coastal Union
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh maarufu kama Alikiba ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Coastal Union amekuwa mdhamini mkuu wa timu yake hiyo.

Kiba ambaye anatarajiwa kuichezea timu hiyo kuanzia msimu huu, amekiambia kipindi cha Nyundo ya Baruani cha Azam TV, amekuwa mdhamini wa Coastal kupitia kinywaji chake ya Mo Faya ambacho amekitambulisha sokoni mwaka huu.

"Baada ya kuona kutia nguvu hiyo ya kwamba mimi nitakuwepo katika uchezaji, vile vile nimekuwa mdhamini mkuu kwasababu ya kinywaji changu cha sasa hivi ambacho nimekitoa cha Mo Faya na hii watu watakapokuwa wanakuja kabisa kuangalia mpira wanaweza kupata na vinywaji uwanjani. Vinywaji pia vitakuwa vinauzwa na kusupport Coastal Union," amesema Kiba.

 "Wanajitahidi ni wapambanaji na wanatafuta tittle msimu huu japo kuwa kuna timu kongwe lakini wanasema mpira unadunda. Nimeona ninaweza nikajiunga na Coastal Union kwa sababu ya talent ambayo nipo nayo," ameongeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad