Aliyekabidhiwa Jezi Namba 23 na Cannavaro Afunguka Baada ya Kukadhiwa

Aliyekabidhiwa Jezi Namba 23 na Cannavaro Afunguka Baada ya Kukadhiwa
Baada ya kukabidhiwa jezi namba 23 kutoka kwa Nadir Haroub 'Cannavaro', beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amefunguka machache juu ya kukabidhiwa uzi huo.

Ninja ameeleza kuwa anajisikia faraja zaidi kupata jezi hiyo kutoka kwa Cannavaro ambaye ameichezea Yanga kwa mafanikio makubwa pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya Mawenzi Market ambao ulikuwa maalum kwa kumuaga Cannavaro, Ninja ameahidi kuifanyia makubwa jezi hiyo kama ambavyo mhusika amehitaji.

"Kusema ukweli nimefarijika kupata jezi ambayo ina heshima kubwa Yanga kutokana na mchezaji mwenyewe, nitaipigania kuweza kuipa heshima kama ambavyo Cannavaro ameniagiza ndani ya Uwanja"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad