Ally Hapi Asimulia Alivyopata Tabu Akiwa DC Kinondoni

Ally Hapi Asimulia Alivyopata Tabu Akiwa DC Kinondoni
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally  Salum Hapi ameweka wazi  siri ya kufanikiwa kwake katika siasa na uongozi nchini kuwa ni kujituma huku akisema eneo alilopata tabu katika masuala ya uongozi ni wilaya ya Kinondoni alipokuwa mkuu wa wilaya.

Hapi ametoa kauli hiyo leo Agosti 3, 2018, katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa ajili ya kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya na kuwaaga waliohamishwa vituo vya kazi.

“Nakumbuka kipindi nateuliwa kuwa mkuu wilaya ya kinondoni,nilikuwa nakumbuka kazi nzuri iliyofanywa na Paul Makonda, nilipata tabu sana wengi walisema je, ataweza viatu vya Makonda?, lakini mkuu wa mkoa Makonda hakuniacha katika changamoto na tulijadili pamoja kwa kuangalia vipi vinajenga vipi vinabomoa”amesema Hapi.

Hapi amesema kuwa katika safari ya kuelekea ya kusimamia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayolenga maendeleo ya uchumi wa kati kufikia 2025,atatumia ardhi yenye rutuba mkoani Iringa kuwa ghala la chakula la Taifa, na kutumia misitu kwa ajili kuongeza vyanzo vya mapato mkoani humo.

Agosti 1, 2018 wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Magufuli alisema kuwa angemtengua Hapi kwa sababu wilaya aliyoiongoza imefanya vibaya katika ukusanyaji mapato, lakini amemuacha kwakuwa sehemu kubwa ya viongozi wa Kinondoni walikuwa upinzani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad