Atakaetupa taka feri kukiona chamoto


MANISPAA ya Ilala wamezindua kampeni endelevu ya usafi kwenye Kata ya Kivukoni eneo la Feri jijini Dar es salaam na kutoa agizo kwa wanaochafua mazingira wakikamatwa kutozwa faini sh,50,000. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa na  Ofisa MTENDAJI wa Kata ya Kivukoni  Iginas Maembe katika soko la feri. 

Akizunngumza katika kampeni hiyo Maembe amesema  katika kata hiyo ni kampeni endelevu ya usafi Kama sehemu ya kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya  Sophia Mjema na kuwataka Watendaji na Wenyeviti kushiriki usafi katika maeneo yao. 

"Tumezindua kampeni ya usafi leo tunawaomba wote muwe wasafi kila mmoja amchunge mwezake asiwe mchafuzi wa Mazingira faini yake ni kubwa unaweza ukalipa zaidi ya shilingi 50,000"alisema Maembe. 

Pia ameagiza kila mtu kuwa na chombo chake cha kuifadhi takataka wakiwemo madereva wa daladala wote watii sheria bila kushurutishwa. 

Aliagiza kila daladala ambayo ina shusha abiria katika eneo la Feri Kivukoni  kuweka chombo maalum cha kuifadhi takataka na daladala ambayo itakaidi kukamatwa na kupigwa faini ya papo kwa hapo. 

Aidha pia katika uzinduzi huo timu ya afya Kivukoni na Maofisa wa Manispaa ya Ilala walitoa elimu ya usafi kwa makundi maalum ya Watu wenye ulemavu  madereva wa Bajaj wa Feri pia watii agizo. 

Katika kampeni hiyo ya usafi  ilifanikiwa kuwakamata Dereva na kondakta wake kwa kushindwa kuweka chombo cha kuifadhi taka ndani ya daladala. 

Kwa upande Wake OFISA ELIMU kwa Umma Manispaa Ilala Tabu Shaibu,alisema jukumu la usafi ni la watu wote kuanzia Mtaa had Kata jukumu letu kuakikisha mazingira yanakuwa safi. 

Tabu aliwataka watii sheria na kufuata taratibu zote za usafi ili kata hiyo iweze kuvutia ili na wengine waweze kuiga. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad