Baada ya Simba Kukosolewa Sana Haji Manara Haja na Takwimu Hii

Baada ya Simba Kukosolewa Sana Haji Manara Haja na Takwimu Hii
Siku moja imepita tokea Simba SC wakosolewe na baadhi ya mashabiki kwa kupata ushindi finyu wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, huku wengi wakikosoa timu hiyo kwa kudai kuwa walistahili kupata ushindi mkubwa kutokana na maandalizi yao waliyoyafanya nchini Uturuki.



Baada ya jana Yanga kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, ndio wengi wakaanza kuikosoa tena Simba SC, afisa habari wa Simba SC, Haji Manara sasa ameamua kuja na data mezani kwa wanaoukosoa uchezaji wa Simba SC na matokeo yake.

“Naomba usicoment kabla ya kuperuzi hizo statistics za mechi tatu zilizopita zikihusisha Simba na Ndala!! Wakati fans wa Simba walinuna pamoja na kushinda game zote mbili huku wakiongoza katika umiliki wa mpira kwa kiwango kikubwa”

“Gongowazi wameshangilia sana huku wakizidiwa possession kwa mbali na Mtibwa..nini maana yake? Simba wanataka zaidi ya ushindi, washabiki wake hawaridhiki na points tatu pekee na kuongoza umiliki..wanataka kudominate game kwa zaidi ya 90%”



“Wakati wenzao wanachojua ni piga mbele hata kama kuna mchango wa kusaidiwa tuta la forgery (now wanachangisha ulichonacho)
Nawasihi wachezaji wangu wa Simba hampaswi kushinda peke yake bali mnapaswa kwenda beyond that!!”



“Nyie ndio mngezidiwa possession kama walivyozidiwa Mbute nahisi fans wenu wangewameza!! Nimeweka takwimu za mechi zote na sitarajii kuona mswahili yoyote anabishana na FACTS”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad