Baada ya Zito Kutakiwa Kujisalimisha Polisi ACT-Wazalendo Wamvaa Kangi Lugola

Baada ya Zito Kutakiwa Kujisalimisha Polisi ACT-Wazalendo Wamvaa Kangi Lugola
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kuendelea na majukumu yake kama kawaida kwa kuwa agizo lililotolewa na Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugola halina nguvu kisheria.

Jana Lugola alimtaka Zitto kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi kwa kile kilichoelezwa alitoa maneno ya kichochezi wakati wa mkutano wa hadhara kati yake na Mbunge wa Kilwa Kusini(CUF), Seluiman Bungara 'bwege'.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho,Ado Shaibu ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti Mosi 2018 wakati akizungumza na wanahabari.

Amesema wanasheria wa chama wamelipitia kwa undani tamko hilo la Lugola na kujiridhisha kuwa lina makosa na halina nguvu kisheria.

"Wanasheria wa chama wamejiridhisha pasipo shaka na kugundua kuwa Lugola amekurupuka kutoa tamko lile.Lugola katumia siasa kutoa tamko lile na siyo kufuata sheria.

“Zitto akiitwa kisheria ataenda kuripoti polisi na hatuna sababu ya kuogopa.Zitto ni kiongozi mbunge akiitikia wito huu wa Lugola atakuwa hajiheshimu, "amesema Shaibu.

Shaibu amesema hakuna kosa lolote ambalo Zitto amelitenda katika mkutano ule, lakini Lugola amekuwa na makeke katika kutoa matamko yake.

“Yaani tumetesti mitambo mara moja tu, pale Kilwa kwa kumpandisha jukwaani Zitto imekuwa nongwa watu wanalipuka? Hatuwezi kuvumilia hali hii,"amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad