Baba Jokate Afunguka Mazito Kuhusu Wema na Uwoya

Baba Jokate Afunguka Mazito Kuhusu Wema na Uwoya
Nduguru aliliambia Amani katika mahojiano maalum kwa njia ya simu hivi karibuni kuwa: “Mwanangu, Wema, Uwoya wote wana ndoto za kuwa wanasiasa na viongozi wa umma lakini hawa wawili kuna mambo yanawakosesha fursa.



MAMBO HAYO NI YEPI?

“Mimi Uwoya simfahamu sana, namsikia tu habari zake kwenye magazeti, lakini Wema namfahamu kwa sababu baba yake (marehemu Isack Sepetu) nimefanya naye kazi serikalini. “Matatizo yanayowakosesha nafasi za kufikia ndoto zao hawa watoto yako mengi lakini kubwa kabisa ni kuiacha misingi bora waliyolelewa na wazazi wao.



“Siri kubwa ya kufanikiwa hasa katika kutumikia watu ni kujiheshimu na kufanya mambo kwa siri, siyo kwenda kiholelaholela, unajivunjia heshima mwenyewe,” alisema mzee Ndunguru. Aliongeza kuwashauri Wema na Uwoya kuwa wanapaswa maisha yao yajae ukweli na waepukane kabisa na mienendo ya kuyaonesha mambo yao ya siri hadharani.



AWATAKA WAMUIGE JOKATE

“Nimeona wanampongeza mwanangu kwa kuteuliwa kwake (kuwa DC), na mimi nasema wasiishie kumpongeza tu lakini waige tabia zake. “Jokate ni mwanangu, sisemi ni mkamilifu lakini ni msiri sana, vigumu kumuona kwenye jamii akifanya vitu vya ovyo, tabia hii naomba Wema na Uwoyawaiige itawasaidia kufikia ndoto zao za kuwa viongozi.



MIENENDO YENYE MASHAKA YA WEMA, UWOYA

Mara baada ya Jokate kuchaguliwa katika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya, mijadala ilitawala kuwahusu Wema na Uwoya kuambulia patupu licha ya kuonesha uwezo wa kutumikia wananchi ambapo wengi waliwatilia shaka warembo hao kuwa mienendo yao inatia shaka kupewa nafasi za uongozi.



Miongoni mwa mienendo hiyo ni pamoja na kutokuwa wasiri katika mambo yao ya faragha, tabia zinazoashiria vitendo vya kihuni, ulevi hasa kwa Wema ambaye amekuwa hakaukiwi skendo kwenye vyombo vya habari.


WALIKOTOKA JOKATE, WEMA, UWOYA

Ikumbukwe kwamba Jokate, Wema, Uwoya wote waliibukia katika mashindano ya Miss Tanzania 2006 ambapo Wema alinyakua taji, akafuatiwa na Jokate huku Uwoya akishika nafasi ya tano.

Pamoja na kujishughulisha na mambo mengine ikiwemo biashara na sanaa, wasichana hawa kwa nyakati tofauti walijiingiza katika harakati za kisiasa ambapo Uwoya na Wema walijitosa kuwania ubunge kupitia Viti Maalum Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku Jokate akijitosa kufanya siasa ndani ya umoja wa vijana wa chama hicho katika kitengo cha chipukizi ambacho hata Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliwahi kutumikia kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.



NDUGURU AMTABIRIA MEMA MWANAYE

“Namuona (Jokate) atafika mbali kwa sababu ana malengo mazuri na nchi yake na ndiyo maana hata utendaji wake ni mzuri, hajafika kwenye nafasi hiyo kwa bahati, alimuweka Mungu mbele na kusikiliza ushauri wa wazazi wake,” alisema mzee Nduguru Aliongeza kwa kumtaka mwanaye kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na fikra za kuuchukulia uongozi kama sehemu ya kujipatia kipato badala yake ajitume kuwatumikia watu usiku na mchana.


TABIA NA MIENENDO YA KIMAADILI NI HIZI

Ili Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:

Kutoa Huduma Bora, 2. Utii kwa Serikali, 3. Bidii ya Kazi, 4. Kutoa Huduma Bila Upendeleo, 5. Kufanya Kazi kwa Uadilifu, 6. Kuwajibika kwa Umma, 7. Kuheshimu Sheria, 8. Matumizi sahihi ya Taarifa
KIONGOZI BORA NI YUPI

Kwa mujibu wa John C Maxwell mkufunzi maarufu wa masuala ya uongozi raia wa Marekani anasema: “A leader is one who knows the way, goes the way, and shows the way.” Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba ““Kiongozi ni yule anayejua njia, anakwenda njia hiyo na anaonyesha njia.”

Aidha, sifa nyingine za msingi za mtu kufaa kuwa kiongozi bora ni pamoja na kuwa muwazi, muadilifu, mwenye maono, mjasiri, mwenye subira, mbunifu, muwajibikaji, mwenye kujituma, nidhamu na mfuasi wa mawasilino na walio chini yake.

WEMA, UWOYA WAFANYE NINI?

Pamoja na ushauri ambao wamepewa na mzee Nduguru na baadhi ya mashabiki wao wa kubadilisha mienendo yao ili waweze kutimiza ndoto zao, Amani linawashauri pia kuanza kuyaishi kwa vitendo maisha ya uongozi hata kabla hawajachaguliwa kushika nafasi yoyote, vinginevyo malengo yao hayatafanikiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad