GPL wanaripoti kuwa Bahati alitakiwa kwenda kufanya tamasha kwenye mkutano wa Injili ulioandaliwa na Askofu Wamwabi Francine wa Kanisa la Mlima wa Ushindi Mei, mwaka huu lakini hakutokea.
Kwenye makubaliano ya awali alitakiwa kulipa dopa kimarekani 2000 na alilipwa dola 1000 kama advansi lakini cha ajabu siku zilipokaribia alipotafutwa kwa njia ya simu ili aweze kutumiwa time tu ya ndege Msanii huyo alizima simu.
Bahati ameliambia gazeti la Amani kuwa taarifa sio za kweli na hao waandaaji waliaharibu makubaliano yao wenyewe na halikuwa kosa lake:
Hao watu tulikubaliana kwenye mkataba kwamba ninaenda kuhudumu katika mkutano na siyo tamasha lakini wao wakawa wanatangaza kwamba naenda kwenye tamasha kitu ambacho ni kinyume na makubaliano yetu.
Pia katika mkataba tulikubaliana wao watanitumia tiketi ya ndege lakini hawakutuma, sasa mimi ningeenda kwa muujiza gani? Watanzania wanajua tabia yangu sijawahi kumtapeli mtu maana mimi ni mtumishi wa Mungu“.
Kutokana ana na tuhuma hizo Bahati Bukuku amelogwa Bongo marufuku kuingia Congo lakini pia hata alipotafutwa kwa ajili ya Kurudisha pesa hizo dola 1000 aligoma kabisa.