Barabara ya Chini ya Ardhi ya Kusafirisha Mihadarati Kutoka Mexico Hadi Marekani Yagunduliwa

Barabara ya Chini ya Ardhi ya Kusafirisha Mihadarati Kutoka Mexico Hadi Marekani Yagunduliwa
Mamlaka nchini Marekani zimegundua barabara ya siri ya chini ya ardhi kutoka jengo lililokuwa magahawa wa KFC jimbo la Arizona Marekani kwenda nchini Mexivo.

Barabara hiyo ya umbali wa mita 180 iliyogunduliwa kwenye nyumba moja huko San Luis, inapitia chini ya mpaka hadi kwenye nyumba moja huko San Luis Rio Colorado.

Barabara ya chini ya ardhi ya kusafirisha madawa kutoka Mexico hadi Marekani yagunduliwa Arizona
Walielekezwa kwenda kwa barabara hiyo ya chini ya ardhi baada ya mshukukiwa Ivan Lopez kukamatwa.

Wakati wa kuzuizi cha barabarani mbwa wa polisi wanaripotiwa kuwaelekeza polisi kwenda kwa mifuko miwili yenye madawa ya kulevya ya thamani ya dola milioni moja kwenye gari la Lopez.

Masaibu yaliyompata mfanyabiashara Kisumu baada ya uchaguzi Kenya
Polisi wanasema mifuko hiyo ilikuwa na kilo 118 za dawa ya methamphetamine, gramu 6 za cocaine, kilo 3 za fentanyl na kilo 21 za heroine.


Barabara ya chini ya ardhi ya kusafirisha madawa kutoka Mexico hadi Marekani yagunduliwa Arizona
Polisi walichunguza nyumba ya Lopez ambapo waligundua barabara hiyi ya chini ya ardhi.

Barabara hiyo ilikuwa umbali wa futi 22 chini ya radhi, urefu wa futi 5 na upana wa futi tatu na iliishii kwenda nyumba moja chini ya kitanda nchini Mexico.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad