Barnaba Atoa Povu Kisa Mapenzi

Barnaba Atoa Povu Kisa Mapenzi
Mwalimu na mwanamuziki wa Bongofleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amefunguka na kuwataka watu kuacha kufuatilia maisha yake binafsi anayoyafanya, na badala yake wafuatilie kuhusiana na kazi zake za sanaa anazoendelea kuzifanya.
\

Barnaba ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba ya vijana EATV, baada ya kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii picha za wanawake mbalimbali wakidai wanatoka kimahusiano na Barnaba huku wengine waki-post picha zenye 'tatoo' ya jina lake.

"Mahusiano yangu hayajawahi kusemwa kwenye mitandao na wala sijawahi kuyaweka mtandaoni , na huwa sipendagi kuzungumzia. Kiukweli watu wanaonijua wanadai muziki mzuri nasio hayo mambo hayo ya mtandaoni yanayoendelea", amesema Barnaba.

Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "halafu mwanaume mnashati huwa haongei kila jambo mengine huwa anakaa kimya tu. Mwanaume mzuri na mwenye maadili huwa hawezi  kuongea vitu vingine ambavyo hata havieleweki. Halafu mambo ya familia yangu nadhani waniachie mimi mwenyewe nadhani hata hayawahusu".

Hii si mara ya kwanza kwa msanii Barnaba kuwakana wanawake ambao anadaiwa kuwa nao kimapenzi kwani mnamo Mei 21, 2018 kupitia kamera za eNewz pia alikana juu ya tuhuma alizozushiwa, na kusema kwamba endapo  siku ataamua kuweka wazi juu ya mahusiano yake basi watu wafahamu kuwa anaoa ama anamvalisha pete ya uchumba mpenzi wake nasio vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad