Ben Pol amefunguka hayo kwenye mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni ambapo amedai kuwa
“Bongo Fleva na yenyewe kama imetetereka hapa katikati, naona kama kuna presha ya kutoa muziki mzuri, kuna presha ya kuwa relevant, kuna presha ya wasanii wachanga kutoka, kuna presha ya vyombo kama taasisi kumekuwa na presha ambao ndio walezi wetu,“amesema Ben Pol na kuwazungumzia BASATA.
“BASATA ni chombo na chombo pia kinaongozwa na binadmu, hata tukikataa hatuwezi kujikataa kuwa sisi ni binadamu wote sisi ni binadamu. Kunaweza kuwa na makosa ya kibinadamu pia taasisi yoyote au chombo chochote kwa sababu kinaongozwa na binadamu kinaweza kikawa na makosa ya kibinadamu. Naheshimu namna ambavyo wanasimamia na wanapigania sanaa yetu lakini sote ni binadamu.“amemaliza Ben Pol.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakilituhumu Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwa limekuwa likiwakandamiza kwenye kazi zao badala ya kuwasaidia kama wanavyopaswa kufanya.