Beyonce na Jay Z Watoa Bilioni 2 Kusaidia Wanafunzi Marekani

Beyonce na Jay Z watoa bilioni 2 kusaidia wanafunzi Marekani
Couple yenye nguvu kubwa ulimwenguni, Beyonce na mumewe Jay Z wametoa kiasi cha fedha kutoka kwenye ziara yao ya On The Run II.

Wawili hao wametoa kiasi cha dola milioni moja ambazo ni zaidi ya bilioni 2.2 za kitanzania ili kuwalipia wanafunzi 11 kusoma bure katika vyuo vya Marekani.  Taarifa hiyo waliitoa Queen Bey na Jay Jumapili iliyopita kwenye tour yao huko mjini Atlanta, Georgia.

Fedha hizo zitamgharamia mwanafunzi mmoja mmoja kutoka katika miji 11 ambayo ziara yao hiyo imepita.

Kwa mujibu wa taarifa za za vyombo vya habari nchini humo, kimetaja miji hiyo ambayo wanafunzi wake watanufaika na msaada huo ni Atlanta, Orlando, Miami, Arlington, New Orleans, Houston, Phoenix, Los Angeles, San Diego, Santa Clara na Seattle.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad