Bobi Wine Aiajiri Kampuni ya Mawakili Kutoka Marekani Kumuakilisha Kwenye Kesi

Bobi Wine aiajiri kampuni ya mawakili kutoka Marekani kumuakilisha kwenye kesi
Mbunge asiye na chama nchini Uganda Bobi Wine ambaye anazuiliwa kwa mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria ameiajiri kampuni ya mawakili ya Marekani kumwakilisha kwenye kesi, kwa mujibu wa wakili Robert Amsterdam.

Bw Amsterdam anasema kukamatwa mteja wake kumechochewa kisiasa na ni kitendo cha dhuluma na kuongeza kuwa ameteswa akiwa kizuizini.

Jeshi ambalo ndilo linamzuia Wine linasema kuwa hajateswa na Rais Yoweri Museveni ametupilia mbali madai hayo na kuzitaja kuwa bahari za uongo.

Amezuiliwa tangu wiki iliyopita pamoja na wabunge wengine kadhaaa. Walikuwa kwenye kampeni kali eneo la Arua kaskazini mwa nchi. Wine anaratarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi.

Amsterdam anasema kuwa Marekani inastahili kuwawekea vikwazo maafisa wa Uganda akiongeza kuwa ni lazima wafahamu kuwa kuna majibu kwa ukiukaji huu wa haki za binadamu.

Sheria za Marekani zinazofahamika kama Magnitsky zinaruhussu bunge la Congress kuwawekea vikwazo wale wanaokiuka haki za binadamu popote pale duniani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad