Bobi Wine Hali Mbaya Alazwa Hospitali

Bobi Wine Hali Mbaya Alazwa Hospitali
Mbunge wa Kyaddondo Mashariki Robert Kyagulanyi amelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Lubaga tangu Jumatatu usiku.

Mbunge huyo maarufu kwa jina la kisanii la Bobi Wine ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini aliachiwa Jumatatu kwa adhamana katika Mahakama Kuu ya wilaya ya Gulu mbele ya Jaji Stephen Mubiru baada ya kushikiliwa kwa wiki mbili katika gereza la kijeshi la Makindye.

Wabunge wengine akiwemo mteule wa Manispaa ya Arua Kassiano Wadri, Paul Mwiru wa Jinja Mashariki, Gerald Karuhanga wa Ntungamo, wanasiasa na wanaharakati waliokuwa wakishikiliwa pamoja na Bobi Wine waliachiwa pia kwa dhamana.

Bobi Wine ambaye aliondoka katika mji wa Gulu kwa gari la kubeba wagonjwa aliwasili Hospitali ya Lubaga saa 4 usiku. Kundi la waendesha boda boda na msafara wa polisi vilimsindikiza hadi hospitalini.

Kuwasili kwa Bobi Wine katika Hospitali ya Lubaga kuliibua hofu ya usalama kutokana na wafuasi wake kuingia hospitalini hapo wakitumia milango tofauti.

Amelazwa kwenye Wodi Na 1 ambayo iko karibu na alipolazwa Mbunge wa Mityana Francis Zaake, kwa wiki mbili sasa.

Kukamatwa kisha kuteswa kwa wanasiasa wakiwa kizuizini kumeibua malalamiko kutoka ndani nan je ya Uganda wengi wakilaani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad