Bocco Atoa Ahadi ya Kuifungia Simba Mabao Haya

Bocco Atoa Ahadi ya Kuifungia Simba Mabao Haya
MSIMU uliopita mshambuliaji wa Simba, John Bocco alifunga mabao 14 kwenye Ligi Kuu Bara hivyo amesema msimu huu atapambana kuhakikisha anapambana ili afunge zaidi ya hayo.



Bocco ambaye ni moja kati ya washambuliaji warefu Bongo ameweka wazi ishu hiyo baada ya kuongezeka kwa timu kutoka 16 za msimu uliopita hadi 20 msimu huu.



“Msimu huu kwa kweli nimepanga kufunga mabao mengi zaidi ya msimu uliopita ambao nilimaliza nikiwa nayo 14, hivyo nina jukumu kubwa mbele kuhakikisha ninatimiza hilo.



“Tunaiheshimu kila timu ambayo tunakutana nayo kwa kuwa hakuna timu ambayo haijafanya usajili mzuri hata sisi pia tumefanya hivyo tutapambana kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu,” alisema Bocco.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad