Shughuli ya ubomoaji wa majengo ambayo imekuwa ikiendelea Kenya kuondoa majumba yaliyojengwa katika maeneo yaliyotengewa barabara na yaliyo kwenye kingo za mito na chemchemi Ijumaa iliathiri jumba lenye moja ya maduka makuu ya Nakumatt, Ukay Mall.
Ubomoaji wa jengo hilo umeanza mapema asubuhi.
Ukay Centre ambayo wakati mwingine hufahamika kama Ukay Mall ni jumba linalopatikana katika mtaa wa Westlands, Kenya na thamani yake inakadiriwa kuwa karibu Kshs1bn.
Mgahawa wa Java wabomolewa Nairobi
Wakaazi waokota kilichosalia katika bomoa bomoa Kibera
Ubomoaji wa jumba hilo umetokea siku moja baada ya Mahakama Kuu kukosa kutoa agizo la kuzuia kubomolewa kwake.
Jumba hilo limejengwa karibu na mto Kinagare na zilifurika maji wakati wa mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2016.
Nakumatt Ukay
Ubomoaji wa majengo unafanywa na Mamlaka ya Taifa ya Mazingira Kenya (Nema).
Serikali ya kaunti ya jiji la Nairobi pia imekuwa ikibomoa majengo yaliyojengwa bila idhini.
Ubomoaji
Alhamisi, Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali yake haitalegeza msimamo wake katika kubomoa majengo yaliyojengwa meneo ya chemchemi au katika ardhi ya umma iliyonyakuliwa.