BREAKING: Mgombea udiwani wa Chadema Arusha achomwa kisu


Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Kata ya Kaloleni jijini hapa na msaidizi wake wamechomwa visu na kukatwa mapanga. 

Kwa mujibu wa vyanzo jijini hapa, tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia jana kwenye kata hiyo ambapo watuhumiwa na tukio hilo hawakufahamika mara moja huku wakihusishwa na kikundi cha chama. 

Ilielezwa kuwa, mara baada ya kuvamiwa, wawili hao walichomwa visu kisha kukatwa mapanga ambapo hali zao zilikuwa mbaya huku mgombea udiwani akizirai. 

Taarifa hizo zilithibitishwa na Polisi na kwamba zoezi la kuwasaka wahalifu linaendelea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad