Mtoto wa marehemu aitwaye Abuu amethibitisha kifo cha baba yake.
Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram.
“R.I.P King Majuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana katika Tasnia ya Comedy Tanzania, sisi wanao, tutakukumbuka kwa kazi zako, upendo wako, tabasamu lako Daima milele, tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani Mzee wetu,” amendika Joti.
Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma Shule Msambwini, mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10.
Hivi karibuni Mzee Majuto alisafirishwa na kupelekwa nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejea nchini ambapo alipelekwa Muhimbili kuendelea na tiba yake.
Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.