CAF Yaridhishwa na Maandalizi ya Tanzania

CAF Yaridhishwa na Maandalizi ya Tanzania
Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamad Ahmad, amesema, ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).


Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamad Ahmad, katikati ni Waziri mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 27, 2018) wakati akizungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.

Kwa upande wake,Waziri Mkuu WAZIRI amesema mechi zoteza michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es Salaam.mashindano

"Tupo katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK Park utatumika kwa mazoezi."

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao wengi wao ni wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad