Calisah Kuja na Vidonge vya Kung'alisha Ngozi

Calisah Kuja na Vidonge vya Kung'alisha Ngozi
BAADA ya ‘kutrend’ na ishu ya kuwapa mimba wanawake 25, mwanamitindo maarufu Bongo, Calisah Abdulhamid, ameibuka na ishu nyingine kuwa yupo mbioni kufungua duka la vidonge vya kung’arisha ngozi kwa wanawake.

Akizungumza na Vijistori Mitandaoni, Calisah ambaye amehusishwa mara kibao kubadili ngozi yake na kuwa mweupe, alisema weupe wake umetokana na AC za magari na si vinginevyo kama watu wanavyoeneza.

“Hapana sijawahi badili rangi ya mwili wangu, mimi ndo nipo hivihivi tangu zamani, kubadili ngozi kwanza ni mambo ya kike ambayo sijawahi kufanya hivyo, hizi ni AC tu za magari halafu mimi ni mtu ambaye naamini sana kwenye muonekano wa kiume ndiyo mana hata nafanya mazoezi, kwa hiyo sijawahi kufanya hivyo kwa sababu hata familia yangu ni ya watu weupe,” alisema Calisah na kuongeza;

“Kwanza nipo mbioni kufungua duka la dawa za vidonge vya kung’arisha ngozi kwa wanawake ambapo Bongo hii hakuna, mimi ndiyo nimeagiza pekee na nitakuwa naziuza ofisini kwangu,” alimaliza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad