Chadema Kumburuza Waitara Kamati ya Maadili

Chadema kumburuza Waitara kamati ya maadili
Chama cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) kimempeleka Mwita Waitara.kwenye kamati ya maadili ya jimbo la Ukonga, kikimtuhumu kusambaza ujumbe wa chuki.

Waitara ni mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo, awali alikuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema kabla ya kuhamia chama tawala ambako alipitishwa tena kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza leo Jumatano, Agosti 29, 2018 mkurugenzi wa operesheni na mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema sababu ya kumpeleka kwenye kamati hiyo ni kutokana na madai ya kuhamasisha vurugu kupitia mtandao wa kijamii.

Amesema kwa kutumia simu yake ya kiganjani Agosti 26, 2018,  Waitara aliandika kwamba watu wa kabila lake yaani Wakurya hususan ukoo wa Wairegi wanoe mapanga yao na kumwaga damu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi jimbo la Ukonga.

Amesema Waitara alitumia lugha ya Kiswahili na Kikurya kuandika ujumbe huo.

Katika maelezo yake Kigaila amesema  Chadema wameitaka kamati ya maadili, kumuita na kumhoji Waitara.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ni msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad