China Inafanya Mazoezi ya Kushambulia Vituo vya Marekani

China Inafanya Mazoezi ya Kushambulia Vituo vya Marekani
Kuna uwezekano kuwa jeshi la China linafanya mazoezi ya kushambuia vituo vya Marekani na vya washirika huko Pacific, kwa mujibu kwa makao makuu ya ulinzi ya Marekani.

Ripoti ya kila mwaka kwa Congress inasema kuwa China inaongeza uwezo wake wa kupeleka ndege za kivita kwenye visiwa vyake vya baharini.

Ripoti hiyo inazungumzia kuongezeka uwezo wa kijeshi wa China ikiwemo bajeti kubwa ya dola bilioni 190, thuluthi ya ile ya Marekani.

Onyo kuhusu mashambulizi ya angani ni moja ya malengo ya kijeshi na kiuchumi ya China.

"Kwa miaka mitatua iliyopita PLA [People's Liberation Army] limepanua maeneo yake ya kufanyia mazoezi bahrini, na kupata ujuzi wa maeneo muhimu ya baharini na kuna uwezekazo kuwa linafanya mazoezi kushambulia vituo vya Marekani na vya washirika," ripoti hiyo ilisema.

Marekani yaionya China kuhusu visiwa bandia baharini
Inaendelea kusema kuwa haijulikani ni kipi China inataka kudhibitisha kwa kufanya mazoezi kama hayo.

"PLA huenda linataka kuonyesha kuwa lina uwezo wa kushambulia Marekani na vikosi washirika kwenye kambi za jeshi magharibi mwa bahari ya Pacific ikiwemo Guam," ripoti hiyo iliongeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad