Wakati msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiendelea na matibabu Afrika Kusini, daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya koo, masikio na pua wa Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Muhas), Godlove Mfuko ameelezea ugonjwa huo.
Dimpoz anasumbuliwa na koo tatizo ambalo limewahi pia kumpata rapa mkongwe aliyewahi kutamba na bendi za Extra Bongo na Twanga Pepeta, Grayson Semsekwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Akifafanua kuhusu ugonjwa huo ambao kitaalamu unaitwa ‘Dysphagia’ alisema husababisha mtu ashindwe kumeza chakula au vimiminika kwa urahisi au kupata maumivu katika koo.
Alisema tatizo hilo ambalo limewahi kuwapa wanamuziki maarufu kama Mariah Carey, Linda Ronstadt na Lauryn Hill huanza taratibu kwa mtu kushindwa kumeza chakula au kumiminika au kupata maumivu iwapo tatizo hilo limefikia katika hatua za juu.
“Matatizo yanayosababisha chakula kisipite kutoka kwenye koo kwenda tumboni ni mengi. Yapo ya kuziba kwa mfumo wa kupitisha chakula yaani esophagus, uvimbe au saratani,” alisema.
Akizungumzia matibabu ya ugonjwa huo, Dk Mfuko alisema kama uvimbe umeshakuwa mkubwa, pamoja na matibabu lazima kunakuwa na huduma ya upasuaji.
“Mwanzoni tunaangalia uvimbe ni wa aina gani, tunafanya kipimo kinachoitwa endoscopy lakini kama hatuwezi kuona vizuri tunafanya CT Scan ambayo inaweza kuona vizuri zaidi kujua uvimbe umeenda mpaka wapi,” alisema Dk Mfuko.
“Kinyama kidogo hupimwa maabara, kama ni saratani lazima itolewe kwa upasuaji kama ni uvimbe wa kawaida kwenye umio, tunakata ili mtu aendelee kumeza chakula vizuri.”
Alisema moja ya matibabu wanayopewa wagonjwa hao ni pamoja na kutoboa tumbo ili chakula kiende moja kwa moja tumboni pasipo kupitia kwenye koo.
Alipoulizwa kuhusu ukubwa wa tatizo hilo hapa nchini alisema, “Sina takwimu halisi nimekuwa daktari bingwa kwa miaka mitatu sasa wagonjwa wengi niliokutana nao ni watu wazima kuanzia miaka 50. Ni ngumu kuona mtoto au umri mdogo.”
Dk Mfuko alisema Ommy Dimpoz anaweza kuendelea na muziki iwapo tu tatizo lake lilikuwa katika mfumo wa chakula pekee.
Alibainisha kuwa koo la chakula halina uhusiano na la sauti ambalo kazi yake nyingine ni kupitisha hewa.
“Ugonjwa huu unaweza kuziba sehemu tatu, kwenye koo mpaka kifua au mpaka tumbo, kwa hivyo mara nyingi kama mgonjwa anakuwa anashindwa kumeza chakula huwa hana matatizo katika koo la sauti.”
Dk Mfuko anasema koo la sauti lina kazi mbili kupumua na kutoa sauti.
Simulizi ya Semsekwa
Semsekwa alisema alilazimika kukaa benchi miaka mitano ili kujiuguza koo baada ya kupewa masharti ya kutoimba, kunywa pombe na kuvuta sigara.
Semsekwa ambaye kwa sasa anaitumikia bendi ya Tamba Stars, alifanyiwa upasuaji wa koo na kupewa masharti ya kukaa mwaka mzima bila kuimba, kunywa pombe, kuvuta sigara na kushiriki tendo la ndoa.
Daktari Afunguka Chanzo cha Ugonjwa Unaomsumbua Ommy Dimpoz
2
August 30, 2018
Tags
Inawezekana Dimpoz ana ugonjwa mwingine ambao hataki kuutaja badala yake anasema kapewa sumu, maana watu wenye magonjwa sugu huwa wanasema wamerogwa au wamepewa sumu kama yule Sam wa ukweli alisema karogwa kumbe alikuwa na ikimwi
ReplyDeleteDimpoz anaujua ugonjwa sugu unamsumbua na ndiyo maana hana amani na ndiyo maana kapungua sana kimwili ukweli mwisho wa siku utajulikana tu
ReplyDelete