Dayna Nyange aweka wazi wasanii wa kike Bongo hawapendani


Dayna Nyange amesema kuwa wasanii wengi wa kike Bongo wanachukiana na hawapendi kuona mafanikio ya wanawake wengine.

Msanii huyo akiongea na kipindi cha Refresh cha Wasafi TV, amesema anawaona kama masnitch kwa jinsi wanachukuliana tofauti katika maisha yao.

Dayna ameongeza kuwa dalili za kichawi sio kwamba mtu uwe unapaa tu na kuloga ila hata ukiwa na roho ya Kukunja na kuzuia mafanikio ya watu wengine ni sehemu nyingine ya kuonekana mchawi kwenye maisha yako.

Muimbaji huyo kwa sasa ameachia wimbo wake mpya 'Salama' ambapo ngoma imetayarishwa na Mr T Touch wakati video imeongozwa na Kwetu Studio.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad