Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesema kuwa ameweka mkakati wa kuunganisha sekta ya kilimo na viwanda mkoani humo ili mazao yanayozalishwa kwa wingi yasaidie kwenye kulisha na kuanzisha viwanda mkoani humo ili kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi kupitia sekta hiyo.
Akizungumza leo Asubuhi Hapi amesema kuwa Mkoa wa Iringa karibu asilimia 80 ya wakazi wake wanashiriki katika kilimo hivyo kwa mkakati huo itasaidia kuwakomboa wakulima wengi kujikwamua kiuchumi na kujiingizia kipato.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Iringa ni moja kati ya mikoa ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula ikiwemo Mahindi, Pareto, pamoja na mazao mengine yakiwemo ya mbao na matunda hivyo uanzishwaji wa viwanda vya uchakataji mazao hao utasaidia kuinua sekta ya viwanda.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa mpaka sasa wana viwanda takribani 2663,lakini wana mpango wa kuanzisha viwanda vingine vipya iwe juu kabisa na vyote vikiwa vinatumia malighafi kutoka mkoani Iringa.
Rais Magufuli Machi 11, akizindua kiwanda cha kufua vyuma cha Kahama mkoani Shinyanga alimwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha wamiliki wa viwanda vya ndani wanaajiri wazawa.