DC wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na Kazimzumbwi wilayani humo kuondoka mara moja kabla hajatumia nguvu.
Akiwa ndani ya msitu wa Ruvu Kusini Jokate amezindua operesheni ya siku 6 ya kuwaondoa wavamizi na kuipa jila la “Operesheni Jokate”.
Jokate ameyafanya hayo leo Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa Ruvu Kusini ambako alienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi waliopo humo.
Amesema lengo lake ni kuwasaka na kuwaondoa wavamizi ambao hawataki kufuata sheria na utaratibu wa hifadhi ya misitu katika msitu wa Ruvu Kusini.T
Jokate nia yako ni njema. Ila labda ungefanya hivi.:shirikiana na idara ya ardhi ili wakupe eneo la makazi au shughuli inayofaa kwa watu hao wavamizi. Kisha wape hata wiki 12 hivi za kuhamia huko ulikowaelekeza. Hiyo itawapa muda wa kukamilisha makazi mapya, kisha hata utamapotumia nguvu dhidi wa ya waliokaidi itakuwa imeeleweka. Kumbuka kama utawaondoa bila kuwaambia waende wapi, utakuwa bado hunamaliza matatizo, ila tu utakusaidia umesolve shida moja na kubaki shida nyingine ya displacement na homelessness.
ReplyDelete