Dereva wa Mbunge Bobi Wine Afariki kwa Kupigwa Risasi Kwenye Kampeni

 Dereva wa Mbunge Bobi Wine Afariki kwa Kupigwa Risasi Kwenye Kampeni
Mbunge wa Jimbo la Kyaddondo Mashariki nchini Uganda ambaye pia ni msanii wa muziki nchini humo, Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine, ameripoti kuwa dereva wake, Yasiin Kawuma,  ameuawa kwa kupigwa risasi wakati wakiwa kwenye kampeni huko Arua jana Jumatatu, Agosti 13, 2018, jioni.

Wakati wa tukio, viongozi kadhaa wa upinzani walikuwa kwenye kampeni wakimsapoti mgombea huru Kassiano Wadri anayegombea ubunge wa Arua baada ya Mbunge Ibrahim Abiriga kuuawa kwa risasi.


Aidha, Bobi Wine amewashutumu polisi kuhusika na tukio hilo na kudai zoezi hilo la kampeni lilikuwa linaenda vizuri hadi pale polisi walipoingilia na kuanza kukwaruzana na wafuasi wa Kassiano Wadrip


Katika Mtaa wa  Dorcus Inzikuru, wafuasi wa Kassiano Wadri Kassiano, mwanasiasa mpinzani, walikuwa wakiandamana mbele ya wafuasa wa Nusura Tiperu, mbomgewa wa chama cha National Resistance Movement (NRM), ambapo baadaye risasi zilianza kurushwa kuwatawanya wafuasi wa Wadri.


Kundi hilo lilijibu mapigo kwa kurusha mawe dhidi ya vikosi vya usalama.

Kyagulanyi ni mmoja wa wanasiasa waliokuwa wakiendesha kampeni kumuunga mkono Wadri ambapo Rais Yoweri Museveni alikuwa akiendesha kampeni kumuunga nkono Tiperu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad