Dogo Janja Sio Muimbaji- Jay Melody

Dogo Janja sio muimbaji"- Jay Melody
Msanii wa kizazi kipya ambaye anafanya vizuri na kibao chake cha 'mikogo sio', Jay Melody amefunguka na kudai, rapa Dogo Janja sio mwanamuziki wa kuimba na ndio maana ameweza kumfunika katika wimbo ambao amemshirikisha.


Jay Melody ametoa ufafanuzi huo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha PLANET BONGO 'PB' kinachorushwa na East Africa Radio hii leo, baada ya watu wengi kutoa malalamiko yao kuwa Janjaroo ameshindwa kuutendea haki wimbo wa 'mikogo sio' kutokana na jinsi anavyoimba.

"Dogo Janja sio muimbaji na ndio maana katika wimbo wangu anaonekana kama hajafanya vizuri, kwasababu yeye alianza na kuchana kipindi alipoingia katika 'game' ndio maana inampa tabu kupita katika maudhui mengine", amesema Jay Melody.

Pamoja na hayo, Jay Melody ameendelea kwa kusema "nimefanya kazi na Dogo Janja kwasababu ya biashara, kutokana na mwenzangu kuwa na watu wengi wanaomfuatilia ndio maana nikaamua kumshirikisha katika wimbo wangu kusudi tuweze kufanya biashara".

Imekuwa kawaida ya baadhi ya wasanii wa kurapu kushindwa kufanya vizuri pindi wanapokuwa wanashirikishwa wimbo na wasanii wa kuimba, kwa kile kinachoelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa inasababishwa na maudhui wanayokutana nayo katika nyakati hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad