Duma afichua siri ya watu kujaa kwenye uzinduzi wa filamu yake


Msanii wa filamu bongo, Daudi Michael maarufu kama 'Duma' amefunguka na kudai sababu kubwa ya yeye kujaza watu wengi katika uzinduzi wa filamu yake mpya ya 'nipe changu', umetokana na nguvu alizojaliwa na Mwenyezi Mungu na wala sio uchawi kama watu wanavyosema. 

Duma amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya watu kushuhudia mamia ya watu waliojitokeza Mliman City siku ya Jumamosi, kutazama filamu hiyo na kusababisha kuzuka minong'ono kwamba huenda ametumia nguvu za kiza kujaza watu. 

"Mimi kuwajaza hawa watu ni nguvu niliyopewa na Mungu, huu ni ufalme niliyopewa na Mungu sio mimi, watu wote hawa wamekuja kwa mapenzi yao kwa Duma. Hakuna uchawi unaotumika kwangu bali ni kufanya kazi tu",amesisitiza Duma. 

Aidha, Duma amesema kupitia kazi yake hiyo, itaweza kuwanyamazisha wale wote waliokuwa wanamwambia kazi yake ni kuongea 

Duma ambaye ameanza kujiuhusisha na masuala ya sanaa mnamo mwaka 2007 amekuwa ni miongoni mwa wasanii wa kiume wasiokwisha kuzungumzwa midomoni mwa watu, kutokana na matukio yake mbalimbali ikiwemo majigambo kuwa yeye ndio msanii bora wa kiume.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad