Esha Buheti Afunguka Ukaribu wake na Ali Kiba na Diamond...Afunguka Kuwahudumia Wote


Mwanadada muigizaji lakini pia mjasiriamali ambaye anajishughulisha na upishi wa chakula na pia akiwa na Saloon yake Esha Boheti amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na kazi zake zote.

Mwanadada huyu amefunguka juu ya changamoto anazozipitia kwenye kazi yake ya uuzaji wa chakula na lusema kuwa “kuna kipindi unaweza kuagiziwa chakula lakini mtu asilipe au mtu anaagiza chakula yuko mbali gharama zote unatakiwa kulipa wewe kwahiyo changamoto kama hizi zinasababisha biashara idorore.

Mbali na kufunguka hayo lakini pia ameongelea kuhusiana na ukaribu wake na Msanii alikiba pamoja na Diamond Platinumz.

Boheti alisema “Mimi namsapoti sana Alikiba lakini kwenye biashara sina utimu kwani hata familia ya Diamond Platinumz ambayo inasemwa ndio wapinzani na Ali mimi naiuzia chakula mfano mama Dangote,dada yake Damond wate nawauzia chakula na tuna urafiki mzuri tu”

Lakini baada ya kuulizwa vipi kuhusu Diamond Alisema : “Mimi na Diamond hatujawahi kukutana na sijawahi kumuuzia chakula changu ila akihitaji chakula ntampelekea popote alipo sitaangalia U timu eti kisa mimi timu Kiba ndo nisiuze chakula hapana”

Alikiba na Diamond wamekuwa katika mchuano kwa muda sasa kwa kulinganishwa ngoma zao na jinsi wanavyofanya kazi zao na ndio maana wamejizolea mashabiki wengi sana Tanzania na hata nje ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad