Faiza Alliy Atema Cheche Kuhusu Tuhuma Zinazomkabili Steve Nyerere

Baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali katika tasnia ya filamu wameona kuwa jambo linaliendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu kumsema Steve Nyerere ni jambo baya na linamkosesha amani yeye na familia yake.

Lakini pia jambo hilo limemfanya Steve ukata tamaa na kupoteza tena ule moyo wa kujitolea kila linapotokea jambo, na ndipo walipoanza kufunguka na kuomba wamuache Steve kumuandama kwa tuhuma za kuwa anakula pesa za rambirambi kweny misiba.

Faiza Ally anasema , wasanii wa bongo movies wameshndea kuelewa umuhimu wa steve na ndio maana tangu tuhuma hizi zianze wamekuwa kimya bila kuongea chochote.Lakini pia yeye anamini kuwa Steve ni mtu muhimu sana katikati yao anaewaunganisha kwa moyo wake tena bila kulipwa wala kuombwa.

Faiza anasema kuwa watu wanasahau kuwa steve amewasaidia mambo mengi tofauti na misiba , amekuwa nao katika harusi, katikakazi na dili nyingi mbalimbali lakini leo hii wanasahau na kukaa wakicheka tu pale wanapoona msanii huyo anatuhumiwa vibaya.

Faiza anawaomba wasanii wote kusimama na kuungana pamoja ili kumtetea na kukanusha tetesi zinamzomkabili Steve Nyerere ili kuendelea kuweka heshima yake.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad