Faiza Ally "Sijaenda Kwenye Msiba Wa Mama Sugu Sababu Alikuwa Hanipendi"


Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa Msanii wa Bongo fleva na Mbunge wa Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi sababu zilizompelekea mpaka kushindwa kuhudhuria msiba wa Mama Mkwe wake.

Siku chache zilizopita Mama mzazi wa Sugu Bi. Desderia Mbilinyi aliaga dunia baada ya kugua kwa muda mrefu ambapo siku ya jana ilifanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Muhimbili hospitali.

Lakini siku ya jana hapo kanisani Faiza hakuonekana kabisa na badala yake alionekana mtoto wake aliyezaa na Sugu hali iliyoibua maswali ya kwanini hakuhudhuria msiba.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Faiza amefunguka kuhusu kutohudhuria Kwenye msiba:

Sijaenda wala sijashiriki Kwenye msiba lakini Sasha ameniwakilisha yupo pale kwa ajili yangu kila mtu akimuona Sasha pale atajua amemuwakilisha Faiza.

Sikujisikia kwenda pale kwa mtu ambaye hajawahi kunipenda na mimi naamini ukienda Kwenye msiba wa mtu ambaye hajawahi kukupenda naamini unaenda kupata dhambi unatakiwa ukifika pale uwe na majonzi na mapenzi kwaiyo sikuhitaji kuwepo sehemu ambayo sijutakiwa kuwepo”.

Faiza amekuwa Kwenye mgogoro wa muda mrefu na Sugu pamoja na Familia yake yote kutokana na malezi ya mtoto wao Sasha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad