Fid Q Amaliza utata Baina yake na Joh Makini

Rapa mkongwe Fid Q amefunguka na kuweka wazi kuwa tungo alizozitumia katika nyimbo yake ya kibiriti, hazimuhusu msanii yoyote yule kama baadhi ya watu wanavyofikiria katika vichwa vyao, bali wimbo huo una muhusu yeye kwa asilimia 100.


Fid Q amebainisha hayo alipokuwa anazungumza na Big Chawa ndani ya kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, baada ya watu kueneza uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wana bifu la chini chini na ndio maana Fid ameamua kumuimba.

"Lahasha wimbo wangu wa kibiriti haumuhusu Joh Makini kwa lolote lile bali ni nyimbo ambayo inanihusu mimi asilimia 100, ambapo naongelea watu ambao wamekuwa wakiniponda kuhusiana na kazi zangu za kimuziki. Kwa hiyo nyimbo yangu ni makusanyo ya maneno yao pamoja kashfa mbalimbali zilizokuwa zinanilenga mimi moja kwa moja na wala sijamsema msanii mwenzangu, amesema Fid Q.

Mbali na hilo, Fid Q amedai kinachofanya watu wanamlinganisha yeye na Joh Makini ni kutokana na kazi zao nzuri ambazo zilikuwa za ushindani tokea walipoanza game ya kurapu.

Hii si mara ya kwanza kwa marapa hao wawili kuhisiwa wana bifu baina yao, na hayo yote yanatokona na wao kuwa washindani katika uwanja huo wa kurapu huku wengine wakiwashindanisha kwa vitu

EATV

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad