FIFA Yamfungia Rais wa Soka la Palestina Kisa Jezi ya Messi

FIFA Yamfungia Rais wa Soka la Palestina Kisa Jezi ya Messi
Shirikisho la soka duniani FIFA limemfungia Rais wa shirikisho la soka nchini Palestina (PFA), Jibril Rajoub kwa miezi 12 kutojihusisha na soka baada ya kukiuka kifungu cha 53 cha sheria za shirikisho hilo ikiwemo kueneza chuki na vurugu.


Kiongozi huyo amekutwa na hatia ya kuwahamasisha mashabiki wa soka kuichoma jezi pamoja na picha za mchezaji wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi.

Maneno hayo aliyatamka kuelekea mchezo wa kirafiki kati ya Israel na Argentina, 9 Juni 2018 mjini Jerusalem ambapo baadae mchezo huo uliahirishwa.

Jibril Rajoub pia ametozwa faini ya CHF 20,000 fedha ya Uswisi ambayo ni sawa na takribani Sh 46.3 millioni za kitanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya FIFA, kiongozi huyo wa juu wa soka nchini Palestina hatohudhuria mechi yoyote rasmi ya soka kwa kipindi cha miaka 12 ikiwa ni pamoja na kutoonekana katika shughuli za vyombo vya habari uwanjani au siku ambazo michezo hufanyika.

Kiongozi huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Olympic nchini Palestina alichaguliwa kuwa Rais wa shirikisho la soka la nchini humo tangu mwaka 2006

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad