Gali Lililokuwa Linasafirisha Bangi Lapinduka Dereva Asakwa

Gali Lililokuwa Linasafirisha Bangi Lapinduka Dereva Asakwa
JESHI la Polisi mkoani Pwani, linamsaka dereva aliyefahamika kwa jina la Moshi Ramadhan Malinganya, mkazi wa Kisarawe kwa tuhuma za kusafirisha bangi misokoto 193, katika gari alilokuwa akiliendesha.



Kwenye gari hilo pia kumekutwa ndoo ndogo mbili za lita kumi, zenye bangi na kiroba kidogo chenye mbegu za bangi kilo mbili, zilizokuwa zimefichwa kwenye buti.



Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kisarawe, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna, ambaye anasubiri makabidhiano kuhamia Mwanza kikazi, amesema mtuhumiwa ametoroka baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka wakati akiwakimbia polisi.

Kamanda Shanna ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana, Agosti 21, majira ya saa 3:30 usiku eneo la shule ya sekondari Minaki, ambapo mtuhumiwa alikuwa anaendesha gari yenye namba za usajili T 801 AAF aina ya Toyota Mark II.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad