Msanii wa bongo fleva na 'video vixen' nchini, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kudai yeye ni miongoni mwa wasanii wanaoweza ku-hit kwa wimbo mmoja mwaka mzima bila ya kutoa kazi nyingine mpya, kama anavyofanya Alikiba.
Gigy amebainisha hayo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv kuhusiana na muziki wake, ambapo amesema hapendi kutoa wimbo 'back to back' kwa madai anaweza akaharibu 'brand' yake.
"Siku si nyingi nakaribia kuachia kazi yangu mpya, watu wakae tayari naamini wimbo wangu utatingisha kinoma. Sipendi kutoa ngoma mpya mfululizo kwasababu huwa napenda kujikuta Alikiba kidogo, maana ninaweza ku-hit bila ya kutoa ngoma mwaka mzima", amesema Gigy.
Mbali na hilo, Gigy amekuwa na maoni ya tofauti na wasanii wenzake ambao kwa sasa wanaamini katika kuekeza kwenye albamu kuliko na kuacha wimbo mmoja mmoja.
"Sio kila msanii atakuwa na ubavu wa kuingia studio na kurekodi nyimbo 10 ili atengeneze albamu, kwangu mimi watu watasubiri sana katika hilo ila kama watu wanataka kuni-enjoy basi waendelee kunisikiliza kwenye 'single' moja moja, kwa maana sina hiyo pesa ya kutengeneza albamu kiukweli, halafu siwezi kujifungia studio muda wote kufanya kazi wakati mwanangu ananitegemea", amesisitiza Gigy.
Julai 7, 2018 ndio mara ya mwisho kwa msanii Gigy Money kuacha kibao chake kipya mtandaoni kinachokwenda kwa jina la 'Kiki ni Gigy' aliomshirikisha msanii Whozu pamoja na Sanja ambapo hadi sasa unajumla ya watu waliotazama takribani laki 5.