Goodluck Gozbert: Natumia Akili Zangu za Ndani

Goodluck Gozbert:  Natumia Akili Zangu za Ndani
Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Goodluck Gozbert amefanikiwa kuwatia nguvu na ujasiri baadhi ya watu waliokwisha kata tamaa na maisha, kupitia tungo za mashairi ya wimbo wake mpya ulioupatia jina la 'Nipe', aliouachia usiku wa kuamkia leo.

Kupitia wimbo huo, Goodluck amezungumza mengi kuhusiana na hali ya maisha ya sasa ambayo, wengi wao huwa wanakatishwa tamaa za kutokana na hali ya maisha wanayokumbana nayo katika kipindi kigumu kwa namna moja ama nyingine.

"Hata kama nikiwa sina chakula isinifanye kusahau, ulinilisha nikasaza na hata kama sina mavazi isinifanye ni kufuru na kusahau umeniweka hai, maana wapo marafiki wanaokosa kula na kuvaa na wala hawalalamiki wanashukuru tu", Goodluck ameimba katika mashairi ya wimbo huo na kuongeza.

Mimi nimekupa nini baba cha kunipa kibali kwa kunipa siku zilizofurahisha, tabu kidogo usinifanye ni kakusahau, umeshatenda mengi nikiwa hapa. Kuna nyakati nadhani hii dunia ni ushindani, natumia hadi akili zangu za ndani ila bado nashindwa kuendelea."

Goodluck ni miongoni mwa wasanii wanalioweza kuteka akili za watanzania wengi kutokana na tungo zake zilizojaa uhalisia wa maisha licha ya kuwa anazungumzia masuala ya kidini na kujikuta nyimbo zake zikipigwa hata katika sherehe ambazo si za kidini.

Itakumbukwa mnamo Aprili 03, 2018, Rais Dkt. John Magufuli alishindwa kujizuia mara baada ya kusikia wimbo wa 'Hauwezi Kushindana' wa msanii huyo ukipigwa katika ghafla ya uzinduzi wa mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi 2, na kuomba urudiwe kwa mara nyingine tena kutokana na ujumbe mzuri uliokuwemo ndani yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad