Hadhi Niliyonayo Siwezi Kutafuta Kiki kwa Watoto Mitandaoni- Ray C

Hadhi Niliyonayo Siwezi Kutafuta Kiki kwa Watoto Mitandaoni- Ray C
Mwanamuziki mkongwe wa kike bongo ambaye aliwahi kutikisa Afrika Mashariki kwa sauti yake na kiuno chake laini, Ray C, amefunguka na kudai hadhi aliyokuwa nayo hawezi kutafuta kiki kwa watoto wadogo mitandaoni, kama wanavyomfikiria baadhi ya watu.

Ray C amefafanua hayo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv baada ya yeye kuwakosoa baadhi ya wasanii chipukizi walioingia kwenye sanaa ya muziki, bila ya kufahamu maana halisi ya sanaa na kupelekea kuishua hadhi kutokana na baadhi ya mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya ndivyo sivyo.

"Ukiona nimeongea kitu mtandaoni basi ujue kimenigusa kwa namna moja ama nyingine, mimi siwezi kutafuta umaarufu kupitia migongo ya watu. Nina jina kubwa sana na wala sihitaji kiki wala chochote  maana nikipita sehemu yoyote watu wanafahamu kuwa mimi ni Ray C", amesema Ray C.

Pamoja na hayo, Ray C ameendelea kwa kusema "ningekuwa sina jina ningesema 'yes' natafuta kiki nitoke au nipate umaarufu, nimeshafanya mambo makubwa sana kwenye huu muziki wa Tanzania, sihitaji kiki kutumia mtu maana hawa watoto ni wajuzi tu".

Mbali na hilo, Ray C amesema uwepo wa utandawazi umewafanya wasanii wa kizazi kipya kupenda kufanya muziki wakiwa nusu utupu ili kusudi  waweze kupendwa zaidi, jambo ambalo linapelekea muziki huo kukosa thamani na heshima kama ulivyokuwa enzi za miaka ya nyuma ambapo mtu alikuwa haoni aibu kukaa na mzazi wake kuangalia muziki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad