"Hakuna Mwenye Uhakika na Cheo Chake"- Magufuli

"Hakuna mwenye uhakika na cheo chake"- Magufuli
Rais Dkt. John Magufuli amesema hakuna mwenye uhakika wa cheo katika serikali ya awamu ya tano kwani hata yeye mwenye hana uhakika kama atakuwa Rais wa muda wote na kuwataka viongozi kushughulika na matatizo ya wananchi mapema na sio kumsubiri yeye kuyatatua.

 Dkt. Magufuli amesema hayo jana Agosti Mosi, 2018 wakati akihutubia mara baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu hafla iliyofanyikia Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Hizi kazi sisi sote tumepewa dhamana. Mimi mwenyewe pia nimepewa dhamana, hakuna mwenye uhakika na kazi hizi hata mimi sina uhakika na kazi hizi kwamba nitakuwa Rais wa moja kwa moja. Hii ni kazi ngumu, Hii ni kazi ni ngumu, its terrible job. Leo tu mimi nimeamka saa nane usiku usiku mara IGP ananipigia simu anasema kuna watu wetu wamepata ajali mpakani, kuna mwingine anasema hivi....

Basi na nyinyi mteseke kama mimi ninavyoteseka, ili kusudi tuwasaidie hawa tunaowaongoza. Machozi yao tutakuja kuyalipa hilo hakuna njia ya kukwepa, kama mabaya yamefanyika katika Mkoa wako au wilaya yako. Wewe RC au DC lazima malipo yako utayapata", amesema Rais Magufuli.

Mbali na hilo, Rais Magufuli ameonesha wazi kabisa kuchukuziwa na kitendo cha jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato katika majiji sita.

"Nchi hii ya Tanzania imebarikiwa sana, ina kila kitu. Dodoma ndio inaongoza katika Majiji, Halmashauri, Manispaa n.k Tanzania nzima katika kukusanya fedha nyingi takribani bilioni 24.5. Nashindwa kuelewa ni kwanini jiji la Dar es Salaam lenye wingi wa watu takribani milioni 5.5, linashindwa kufikia malengo yaliyokuwa bilioni 12..Ambapo imeizidi Dodoma kwa 'population'. Sasa unaweza kujua kwamba hapa Dar es Salaam kuna upigaji tena wa nguvu lakini viongozi wapo tu", amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema kwa jinsi hali inavyoendelea wataweka mikakati ya kushusha hadhi ya majiji ambayo yatakuwa yanashindwa kufikisha malengo yake ya kimapato yaliyowekwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad