Halima Mdee Matatizoni Tena, Akamatwa na Polisi


Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  Halima Mdee (Mb) pamoja na viongozi wengine, wanachama na CHADEMA Jimbo la Kawe takriban 13, wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Kawe. 

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amesema Mbunge huyo amekamatwa eneo la Tanganyika Parkers alipokua akizungumza na wananchi wa jimbo lake waliomsimamisha kutaka kumuelezea kero zao. 

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro amesema bado hana taarifa zozote za kushikiliwa kwa Mbunge huyo. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad