Hamisa Mobetto na Zamaradi Hapatoshi Watibuana Kisa Hiki Hapa

Hamisa Mobetto na Zamaradi  Hapatoshi Watibuana Kisa Hiki Hapa
Mwanamitindo Hamissa Mobetto ameonekana na mkosi kwa kila jambo baada ya kutupiwa lawama nzito na Mwanadada Mwanaharakati Zamaradi mketema za kusambaza habari za uongo kuhusu nguo aliyoivaa siku ya 40 ya mtoto wake pamoja na  kuwachangisha pesa watu kwaajili ya kukamilisha shughuli yake huku Zama akidai kuwa sherehe nzima kula, kunywa na kila kitu ameigharamia yeye mwenyewe.

Kupitia akaunti yake ya instagram Zamaradi ameandika waraka mzito na majadiriano ya hamisa mobetto kuhusiano na walichojadiliana kuhusu mshono ambao alishona mwanamama huyo ambapo inadaiwa baada ya kupewa mshono huo akaenda kushona sehemu nyingine.

''tukija kwenye nguo naambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine!! Funny wallah!! Na nimeshangazwa sana na uongo mkubwa wa namna hii, Nimeattach ushahidi hapo juu kuwa MIMI NDIO NIMETUMA HUO MSHONO KWAKE NA SIO YEYE, hakuwa anaufahamu kabla, hata kama kuna roho mbaya mnanipa sio ya kiasi hiko, sasa hapo nani mbaya!? Kutokana na kupishana na muda nikaona nikashone kwingine, na zaidi Swala la kushona popote ni uamuzi, since sio mshono niliochukua kwa mtu nina uhuru wa kuupeleka popote, nina biashara ya duka la nguo nina CATERING ila silazimishi kila ananenijua aje kwangu, na zaidi SIJISIKII VIBAYA riziki inapoenda kwa wengine, sina roho mbaya hiyo, riziki kugawana. Am very dissapointed kiukweli na binaadamu ila nimegundua kinachofanya haya yote sio kwamba wananihofia mimi ila NGUVU YANGU. hata ukinyamanza kimya watu


Baada ya tuhuma hizo nzito Hamisa mobetto aliamua kujibu mapigo kwa kujibu tuhuma hizo pamoja na kuonyesha chat walizotumiana kipindi anaomba ushauri wa nguo anayotaka kuvaa siku hiyo.
Hamisa mobetto aliandika hivi

''First Of All Me sio Mtu wa Kujibishana Na watu insta Ndo maana always nakaaga Kimya .
...... Tangia Nimefungua @mobettostyles Kila siku imekua Jipya .
Secondly sijawahi Sema Popote kuhusu mshono Wa Shughuli yako wala kuandika kwa My page so probably one of your friends kayapeleka sehemu .
My dear ulivyokua hujanialika kwenye shughuli yako nilibezwa kuchekwa kutukanwa and all siku jibu wala ongea popote kwasababu kila mtu ana uhuru wa kuchagua watu atakao .
.
Ulinitafta Tumechagua Mishono umeenda shona kwengine sijawah lalamika my dear wala kusikitika Coz ridhki mafungu saba na kila likuepukalo najuaga huwa lina kheri na Mtu .
.
Hivyo basi kama mtu mzima ungeskia kitu ungenifata na kunambia lakin no umeamua kunichafua just because uweze lala vizuri usiku .

#MniacheJamani #MaanaNadhanSikuMkinitoaRoho #MtafurahiaSana''



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad