Hamissa Mobeto Aliamsha Dude "Daimond Ana Wanawake Milioni 5 Wanaomtaka"

Hamissa Mobeto Aliamsha Dude "Daimond Ana Wanawake Milioni 5 Wanaomtaka"
MWANAMITINDO gumzo Bongo, Hamisa Mobeto ameamua kumwaga mboga kuwa, hata siku moja hawezi kumfanyia mwanamke ubaya katika mitandao ya kijamii kisa kumtaka kimapenzi mzazi mwenziye ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa sababu wapo milioni tano wanaomtamani.

Mobeto aliyafunguka hayo alipoulizwa juu ya ‘kumblock’ msanii wa Bongo Fleva, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ kwenye ukurasa wake wa Instagram kisa amehisi anatoka kimapenzi na Diamond na kusema kuwa, ni kweli alimblock lakini si kwa sababu ya msanii huyo bali alikuwa akipenda kumuongelea vibaya na wakati mwingine kumtukana.

“Kwanza kabisa nilikuwa simjui na hata nilimsahau huyo mtu mwenyewe halafu sikumblock kwa sababu ya Diamond sababu kuna wanawake kama milioni tano wote wanamtamani huyohuyo mtu mmoja sasa kama ndiyo hivyo nitablock wanawake wangapi jamani?

“Yeye (Pretty Kind) kuna maneno machafu na mabaya aliyaongea kuhusu mimi alinichafua sana halafu mimi ni brand simjui nikaona huyu naye katokea wapi? Nikamblock maisha yangu yaendelee kwa sababu wa nini mtu ambaye ananipa kero?” Alisema Mobeto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad