Harmonize Amtaka Mpenzi Wake Azoee Kusikia Ana Michepuko

Harmonize Amtaka Mpenzi Wake Azoee Kusikia Ana Michepuko
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayeendelea kufanya vyema sana  Harmonize amemfungukia mazito mpenzi wake Sarah na kumsisitizia kuwa hana michepuko.

Harmonize ambaye amekuwa Kwenye headlines sana kwa tuhuma za kuchepuka amefunguka na kukataa tuhuma hizo lakini pia amesema Tetesi hizo ni lazima kwa mtu maarufu kama yeye na hata mpenzi wake Sarah lazima azizoee tu:

Harmonize alifunguka hayo nchini Kenya alipokuwa kwenye shoo yake ambapo kwenye mahojiano na Pulselive na kumtaka mzungu wake kuwa mvumilivu:

Sio Kitu Kibaya maanake wivu pia ni Mapenzi, lakini kitu ambacho Sarah inafaa ajue kuwa ukikubali kuwa na Msanii lazima kuna vitu lazima tu ukubaliane navyo tu. Na Life style ya msanii inakaa vipi kuna wengine ni mashabiki na siwezi goma kupiga picha nao maanake bila wao mimi sipo. Kwa hivyo natumai tu anafaa kuelekezwa alafu atajua jinsi ya kuhandle situation kama hizo”.

Sarah na Harmonize waliingia Kwenye mgogoro mkali mapema mwezi huu baada ya Tetesi za Harmonize kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na wanawake kadhaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad