Harmorapa Mzee wa KIKI Alamba Dili NONO la Ubalozi wa Kampuni ya Usafiri

Harmorapa Mzee wa KIKI Alamba dili NONO la ubalozi wa kampuni ya usafiri
Msanii wa muziki Bongo, Harmorapa amepata dili la kuwa balozi wa kampuni ya Moovin inayotoa huduma ya usafiri.

Kampuni hiyo  ya usafiri ya Moovin ilimtangaza rapa Harmorapa pamoja na mtangazaji wa XXL ya Clouds FM jana Jumatatu kuwa mabalozi, tukio ambalo lilifanyika  katika hotel ya Double Tree jijini Dar es salaam

Akiongea baada ya kutangazwa Harmorapa ameishukuru kampuni hiyo kwa kutambua nguvu yake na kuamua kumpatia deal hilo ambalo litamjengea heshima kubwa.

Hapo awali kampuni hiyo ilimtambulisha Madam Ritha wa BSS kuwa balozi wao pia.

Hili ni dili lingine kwa Harmorapa mara baada hapo awali kuwahi kuwa balozi wa kinywaji cha Swala.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad