Shabiki aliyevamia kwenye stage ya Beyonce na Jay Z Jumapili ya August 26,2018 kwenye ziara ya On The Run II(ORT II) amefunguliwa mashtaka na polisi kwa uvamizi ambao ungesababisha madhara kwa watu.
Shabiki huyo anayejulikana kwa jina la Anthony Charles ’26 amepewa onyo kutokana na utovu wa nidhamu kwa tabi yake alioifanya na pia amefunguliwa shtaka la kukusudia kuumiza na kusababisha madhara kwa watu.
Anthony Charles alifanikiwa kuwakwepa walinzi na kupenya hadi kufanikiwa kuingia jukwaani na ndipo alipoanza kuwakimbilia Beyonce na Jay Z, kosa hilo alilolifanya Anthony Charles kama akikutwa na hatia anaweza kufungwa mwaka mmoja jela au kutozwa faini.