Huyu Ndio Mwanamke Pekee Ambaye Yupo Nyuma ya Mafanikio ya Ali Kiba


Jina lake kamili ni Christine Mosha - ila aliamua kutumia jina la 'Seven' kutokana na kufundishwa kuhusu maajabu ya namba 7 - ikiwemo maajabu 7 ya ulimwengu na dhambi 7 kuu katika dunia. Hivyo anaamini namba saba ni yenye nguvu katika maisha yake.

Alizaliwa jijini Nairobi Kenya na kukulia nchini Tanzania. Maisha yake kwenye kioo yalianza kama mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM na baadae mwaka 2009 alitoka na kujiunga na MTV ambapo alihudumu kwa miaka kadhaa kupitia kitengo cha A&R yaani Artiste and Repertoire.

Baadae pia alihudumu katika kampuni kubwa ya muziki duniani Sony kwa muda na kisha baadae kusimamia tawi la Rockstar 4000 kama mkurugenzi wa vipaji na muziki.

Seven ndiye meneja wa kike pekee kwenye game ya Bongo fleva ambapo anasimamia kazi za Ali Kiba pamoja na Ommy Dimpoz kama meneja chini ya Rockstar 4000. Huu ni mwaka wa 7 - Seven anafanya kazi na Kiba, walikutana na mwimbaji huyo katika project ya One 8 wakati huo akiwasimamia wasanii wa Afrika Mashariki.

Ukaribu wao ukaanzia hapo hadi leo amemfanya 'KING Kiba' kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa Afrika na dunia - akifanikiwa kutajwa kwenye tuzo kubwa nje na ndani na kushinda baadhi kama: MTV Europe Music Awards, KTMA, Sound City Awards na nyingine nyingi. Pia kufanya colabo na wasanii wakubwa nje na ndani ya nchi.

Huyu ndio Seven Mosha

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad