Idris Ampa Maneno ya Faraja Hamisa Mobeto


Mchekeshaji Idris Sultan amempongeza Mwanamitindo Hamisa Mobetto kuingia kwenye muziki. Idris amesema yeye anamsapoti Hamisa na anashangazwa na wale wanaomkeli kwa hatua hiyo. 


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Idris ameandika;

"Naomba niwe kati ya wale wa kwanza kukusapoti ili ukija kuanza kuchukua matuzo usitusahau maskini wenzio. Mwanzo sio mwepesi ila kama msimamizi wa mpesa vodacom naweza sema yajayo yanafurahisha. Nitashangaa kuona watu wanakukejeli kwenye hii hatua yako katika upiganaji sijui wanataka ukatembee barabarani unauza nanilii sasa.


"Katika hatua za mafanikio jua sana kuchuja maneno. Kama kweli umedhamiria kufanya mziki basi kazaaa na unatoboa tu kwani hao wengine ni kina nani labda. Wengine tulianza hatukubaliki hata tutoe msaada wanguo zetu tutembee watupu ila unakaza tu na baada ya mda unaanza okota fan mmoja mmoja wawili mwishowe una mamilioni #RefuseToStop"


Jana August 20, 2018 Hamisa Mobetto ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jila na Madam Hero. 


Hamisa ni mrembo mwingine Bongo kujaribu bahati yake kwenye Bongo Fleva baada ya wengine kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo Aunt Ezekiel nakadhalika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad